Suluhisho la Imani za dini: hatua za masuluhisho ya migongano ya kiimani.

faith
Author

Benjamini Mpinga

Published

March 20, 2023

Hatua nne zilizopitiwa na Dini, ili kulinda Imani zao.

Historia ya imani za dini imejumuisha vipindi mbalimbali ambapo imani hizo zimeshindwa na kupata mafanikio katika kuenea na kuheshimiwa na jamii. Baadhi ya watu wamepitia mateso ikiwa ni pamoja na kufungwa, kuuliwa, kutengwa na jamii zao, na kudhihakiwa na kudharauliwa. Makala hii itaangazia hatua kadhaa ambazo imani za dini zimepita hadi kufikia wakati wa sasa. Hatua hizo kuu ziko nne, na hatua ya mwisho yaani ya nne, imeanza kuonesha ishara za watu kuelekea kutimia kwake, kwa sababu hatua hiyo ya nne ni hatua ambayo hainabudi kutokea kwa mujibu wa Unabii.

  • Hostility and antagonism (Utawala).
  • Separatism (Ugawanyo).
  • Pluralism (Upekee kati ya wengi).
  • syncretism (Usawa katika umoja).

Hostility and antignisim.

Hii ni hali ya awali kutokea katika mapambano ya kupigania Imani za dini mbalimbali, mfano sote tunajua hali iliyotokea katika vita ya msalaba (crusaid war), vita vya sunny na shehay kati ya Irani na Iraq, pamoja na vita zingine zinazohusisha mtizamo wa kidini haswa ikipewa jina la Imani. Katika hatua hii watu wengi waliumia na kupoteza maisha pamoja na mali, ila zaidi ikacha jamii nyingi katika uhasama wa wao kwa wao au pengine jamii/taifa moja na wengine. Baada ya njia hii kuonekana kuleta madhara makubwa kwa jamii, palibuniwa njia nyingine ambayo ilikuwa ni hatua ya pili katika kulinda Imani za Dini.

Separatisim.

Kuweka mipaka ya jiografia kwa kuzitenga Imani moja na nyingine kuingiliana kimipaka. Njia hii ilitumika ili kuondoa au kupunguza mauaji na madhara ya mapigano ya Kidini yaliyokuwa na madai ya kutetea Imani. Njia hii ilitekelezwa kwa namna mbalimbali ikiwamo, kuwatenganisha watu wa Imani moja na nyingine kwa kuwapa mipaka ya kuabudu, na sharti la kutokueneza mafundisho yao nje ya mipaka yao waliyopewa. Mfano ni kwamba, mji mmoja ukiwa na imani A, basi mji mwingine unakuwa watu wa Imani B. Hivyo ni marufuku kwa Mtu wa mji A kueneza mafundisho ya Imani yake katika Mji B.

Pluralisim.

Huu ni mfumo wa kuzitambua Dini za imani zote, hususani zile zenye waamini wachache nazo zipewe haki sawa na zile zenye waamini wengi, kwa kigezo kimoja tu, cha kutokuleta mgawanyiko au machafuko katika jamii. Hii ilitoka na na mambo makuu mawili. - Kwamba baada ya kuzichunguza Imani zote jamii iliona kana kwamba kila Imani inafundisha masuala ya kiroho, na kwamba Imani zote zinao kiasi fulani cha ukweli juu ya mambo ya Mungu, hivyo ni vyema kupewa nafasi ili kwa mafundisho ya Imani zote, basi jamii inufaike Kiroho na kubadili tabia za jamii kwa ujumla.

  • Pia hili ilitokana na ukweli kwamba, kiasili mwanadamu hawezi kuwekewa mipaka katika baadhi ya mambo ambayo anayaamini, hivyo ilipoonekana kana kwamba njia ya “Separatisim” inaweza isiwe na suluhisho la Kudumu, ndipo pakabuniwa njia hii ya wingi wa Imani. Ikichagizwa na falsafa ya kwamba, Wingi wa machaguo ni jambo lenye afya kwa jamii, na kwamba kila mtu apewe nafasi ya kuchagua anachokipenda pasipo kulazimishwa au kutishwa. Ndipo dini za imani tofauti tofauti zikawa huru kuendesha shughuli zake katika jamii pasipo kuwekewa mipaka ya jiografia.

Suluhisho hili la kuzitambua na kuziruhusu Dini za Imani zote kuwa na nafasi sawa katika jamii, umekuwa na nafasi kubwa na umeendelea kuchagizwa hadi kizazi cha sasa ambacho tunaishi. Lakini suluhisho hili halitadumu milele, kwa sababu kuu mbili…

Sincrotisim.

Suluhisho hili ni la mwisho na linalenga kuzileta Dini zote za ulimwengu kuwa chini ya mwamvuli mmoja wa Imani. Na limeanza dalili zote za kuja kwake, kwa ishara za kuzifanya Imani za dini mabalimbali kufanya kazi kwa pamoja katika jamii, mfano sio ajabu kuona Makanisa ya madhehebu tufauti yanashirikiana, Kanisa na Msikiti kushirikiana, pia katika hafla za serikali ni wazi sasa kuona Viongozi wa Imani mbalimbali wakijumuika na kila mmoja kupewa nafasi ya kuombea wengine kwa Imani yake, hata kama wengine hawaamini imani hiyo. Njia hii ya kuzifanya Imani za dini zote duniani kuwa pamoja, umeanza kuonesha ishara ya kutokea kwa sababu kuu mbili.

  1. Dunia inahimiza zaidi ushirikiano na mshikamano.
  2. Dalili za unabii wa kitabu cha Ufunuo wa Yohana kutimia.

Dunia inahimiza zaidi ushirikiano na mshikamano.

Kwa sababu ya dunia kuhimiza na kubuni njia mbali mbali za kuunganisha watu kuwa kitu kimoja katika nyanja mbalimbali, ikiwamo Siasa, Uchumi na Elimu ambayo inawaondoa watu kutoka tamaduni zao na kuwa jamii ya ulimwengu. Hivyo moja ya kitu cha mwisho kitakachotafutiwa suluhisho kitakuwa ni Imani za Dini.

Zifuatazo ni baadhi ya Imani na tofauti zake za kimtizamo juu ya Uweza wa kimungu.

  1. ATHEISM — NO GOD
  2. AGNOSTICISM — DO NOT KNOW
  3. ANIMISM — SPIRITS ARE gods
  4. POLYTHEISM — Many gods
  5. DUALISM — two gods (good and bad)
  6. MONOTHEISM — ONE GOD
  7. DEISM — CREATOR CAN NOT CONTROL
  8. THEISM — CREATOR CAN CONTROL
  9. EXISTENTIALISM — EXPERIENCE IS GOD
  10. HUMANISM — MAN IS GOD
  11. RATIONALISM — REASON IS GOD
  12. MATERIALISM — ONLY MATTER IS REAL
  13. MYSTICISM — ONLY SPIRITY IS REAL
  14. MONISM — MATTER & SPIRITY IS ONE
  15. PANTHEISM — ALL IS GOD
  16. PANENTHESM — GOD IS IN ALL

Dalili za unabii wa kitabu cha Ufunuo wa Yohana kutimia.

Kwa kusoma maandiko ya unabii wa kitabu cha Ufunuo wa Yohana katika Biblia, tunaona dalili zote zinazothibitisha kwamba, kwa mwenendo ambao jamii za ulimwenguni zimepitia hadi sasa, basi ni dhari patatokea suluhisho la mwisho lenye lengo la kuzileta Imani zote kuwa katika Mfumo mmoja. Hili litatokana na kigezo kwamba, waamini wa Imani zote wanaamini kwa Mungu, na kwamba Imani zote zinafundisho linalolenga kumjenga mwanadamu katika tabia na Roho. Hivyo imani zitaungana na kutengeneza Imani moja kwa wanadamu wote.

Maswali tunayoweza kujiuliza.

Wakati tunasubiri makala ijayo, ambayo itagusia zaidi katika mada iitwayo “Upekee wa imani kwa Yesu Kristo, isiyoweza kufananishwa na Imani kwa Dini za ulimwengu.”Tujiulize mambo kadhaa ambayo yatatupa mwanga katika makala hiyo.

  1. Je, Imani za dini zote ni za kweli?
  2. Kama zote ni za kweli, mbona zipo tofauti?
  3. Kama sio zote za ukweli, zitakapoungana zitakutengeneza uovu zaidi?
  4. Je, Imani za dini za ulumwengu zikiungana kuwa moja, Itabadilika kuwa imani ya kweli?
  5. Je, kama imani Moja ni ya kweli na zingine zimepotoka, yawezekanaje hii ya kweli kuungana na zilizopotoka?
  6. Ikiwa haitakubali kuungana, unadhani jambo gani litaikabili hiyo Imani moja ambayo itakuwa kinyume na Imani zilizokubali kuwa kitu kimoja?

Katika kuyajibu maswali hayo, tutajumuika kwa mawazo na ushauri, kisha nitakuandalia makala nyingine, itakayoelezea Upekee wa Imani kwa Yesu Kristo, usioweza kufananishwa na imani kwa Dini za ulimwengu.


Stay in touch

If you enjoyed this post, then don't miss out on any future posts by subscribing to my email newsletter

Support my work by sharing the link or by contact through +255 768 596 017.

Share